- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
ZITTO: WAPINZANI WALITENDEWA UGAIDI NA VYOMBO VYA DOLA
MuakilishiTZ
Kiongozi Mkuu wa chama cha Upinzani cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa vyama vya upinzani nchini vimekuwa vikitendewa matendo ya kigaidi kwa miaka mitano na nusa sasa, huku akitolea mifano matendo hayo ya kigaidi ikiwa ni pamoja na wapinzania kufilisiwa mali zao, kufungiwa akauti za benki, kupigwa Risasi akimtolea mfano Tundu Lissu Mbunge wa Zamani wa Singida Mashariki.
Matendo mengine ya kigaidi Zitto ameyataja ni wapinzani kupigwa na kuachwa vilema akitoa mfano viongozi wa juu wa chama chake cha ACT Wazalendo Nassoro Mazrui na Ismail Jussa wote kutoka kule visiwani Zanzibar.
“Sisi Viongozi, Wanachama na Wafuasi wa Vyama vya Upinzani tuliishi kwa mateso sana ndani ya miaka mitano na nusu iliyopita tulifilisiwa mali na kufungiwa akaunti zetu... Ndugu Freeman Mbowe akiwa ni kielelezo cha hili”
“Tulipigwa risasi zaidi ya 30 na mpaka leo hakuna hata uchunguzi dhidi ya vitendo hivyo vya kinyama, Ndugu Tundu Lissu ni kielelezo cha hili, tulibambikiwa kesi na kuhukumiwa Mahakamani (Mimi na mamia ya Viongozi wenzangu wa kisiasa ni kielelezo cha hili)” amesema Zitto hii leo Agosti 8, 2021 visiwani Zanzibar wakati chama hicho kinajiandaa na Mkutano mkuu wa Dharura wa chama hicho hii Leo Jumapili Agosti 8, 2021.
“Mamia ya Wanachama wetu wakipata vilema vya kudumu kwa vipigo (humu kwenye Kamati Kuu tunao kina Jussa na Mazrui), unaweza kusema bila kupepesa maneno kuwa Wapinzani walitendewa ugaidi mkubwa mno na vyombo vya Dola”
“Kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe ni jambo linalokumbusha machungu makubwa sana ya awamu iliyopita, Watu waliofungua mashtaka hayo hawamkomoi Mbowe wala hawatuvunji moyo wa kupambania Tanzania yenye usawa wa kisiasa na kuheshimu utofauti wetu wa mawazo, wanalichelewesha tu Taifa letu kupata Umoja na Maendeleo ya Kiuchumi, wanataka turudi kulekule ambapo hatupaswi kurudi”
“Wito wangu na Viongozi wenzangu kwa ndugu Rais Samia ni kuingilia kati na kumaliza jambo hili la kisiasa kwa njia za kisiasa, Rais asikubali jambo hili, awazuie Wasaidizi wake wanaotaka tuendelee kuishi kama ilivyokuwa ndani ya miaka mitano na nusu iliyopita, tunajua anao uwezo huo, tunajua akitaka anaweza kulizuia jambo hili, tunajua yeye hataki tuendelee kuishi kigaidi” amebsema Zitto