- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: HAKIKISHENI UANDIKISHAJI WA WATOTO WENYE UMRI WA KUANZA ELIMU YA AWALI NA DARASA LA KWANZA UNAKAMILIKA KWA WAKATI
KAGERA: Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais β TAMISEMI anayeshughulikia elimu ya Msingi Bi. Susan Nussu amewataka Maafisa Elimu Kata na Walimu Wakuu kote nchini, kila mmoja ahakikishe uandikishaji wa watoto wote wenye umri wa kuanza Elimu ya Awali na Darasa la Kwanza unafanyika na kukamilika mapema ili kuwapa fursa walimu kuendelea kufundisha.
Bi. Nussu amesema hayo tarehe 20/1/2025 kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Bw. Adolf Nduguru wakati akifunga Mafunzo ya Walimu wa Elimu ya Awali Na Walimu Wakuu katika Chuo cha Ualimu Katoke, Kagera.
Amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 inasi
sitiza utoaji wa elimu bora, kuanzia Elimu ya Awali ambayo ndiyo msingi wa kwanza katika mfumo wa Elimu rasmi kote ulimwenguni. Pia amesema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa Elimu ya Awali ina mchango mkubwa katika makuzi na malezi ya mtoto kiakili, kimwili na kijamii.
Ameongezea kwa kutoa wito kwa wazazi wote wenye wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari wahimizwe kuwapeleka shule wanafunzi hao mepama iwezekanavyo ili kuepuka kukosa mafunzo kabilishi (orientation course) yanayotolewa kama msingi wa ujifunzaji katika ngazi hiyo ya elimu.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Ndugu. Isaya Mbenja amesema anaenda kusimamia utekelezaji wa mafunzo yote yaliyotolewa kwa walimu hao kwa vitendo kwa kuzingatia mahitaji maalumu ili kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu nchini.
Mafunzo hayo yalitolewa na Ofisi ya Rais β TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu yamenufaisha walimu katika halmashauri zote 184 kwa kufundishwa mada mbalimbali zikiwemo nyenzo za kufundishia jumla ya walimu 3,000 wa elimu ya awali ambapo jumla ya washiriki 18,564 wamejengewe uwezo wakiwemo walimu wa elimu ya awali 9670, wakuu wa shule 9,302 kutoka shule 9,302, maafisa elimu wa mikoa 26, wakuu wa divisheni ya elimu msingi 184.