- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MATUMIZI YA BARUTI YAONGEZEKA NCHINI.
DODOMA: Matumizi ya Baruti nchini yameongezeka kutoka wastani wa tani 3,000 kwa mwaka katika miaka ya 1990 hadi kufikia wastani wa tani 26,516.07 kwa mwaka 2024.
Hayo yamesemwa leo Jumatatu Januari 13, 2025 jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani Lwamo wakati akifungua kikao cha kuwajengea uwezo wakaguzi migodi na baruti.
Amesema, kutokana na ongezeko la shughuli za uchimbaji wa madini, utafiti wa mafuta na gesi asilia na ujenzi wa miundombinu mbalimbali, kuongezeka kwa matumizi hayo pia kumepelekea kupanuka kwa biashara ya baruti hapa nchini.
“Matumizi makubwa ya baruti maana yake uchimbaji umeongezeka, hivyo bila udhibiti italeta madhara, kikao hiki ni kujengeana uwezo lengo ni kuhakikisha wachimbaji hawapotezi maisha au kupoteza viungo kwa ajili ya matumizi ya baruti,”amesema Mhandisi Lwamo na kuongeza,
“Ongezeko la uhitaji wa matumizi ya baruti hapa nchini kumepelekea uwepo wa changamoto kadhaa katika usimamizi wake, udhibiti madhubuti ni muhimu, mkadhibiti katika maeneo yenu, itakuwa ni aibu mkaguzi mgodi na baruti eneo lake mtu akapata madhara,”amesema.
Amesema, mpaka sasa kuna zaidi ya bohari (magazine) 231, stoo 493, masanduku ya kuhifadhia baruti zaidi ya 279 yaliyosajiliwa kwa ajili ya kutunzia baruti migodini na maeneo ya biashara ya baruti.
Awali, akimkaribisha mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi Migodi na Mazingira, Hamisi Kamando amesema kumekuwa na matukio mbalimbali ya ajali yanayotokana na kutokuzingatiwa kwa Sheria ya Baruti ya Mwaka 1963, Kanuni za Baruti za Mwaka 1964 na taratibu zingine katika usimamizi wa Baruti.
Naye, Mwanasheria Damian Kaseko amewataka wakaguzi migodi na barutikusimamia sheria, kanuni na sera wanapotekeleza majukumu yao ili kuepusha migogoro na kuwa na mipaka katika utekelezaji wa shughuli zao.