Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 9:40 am

NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI

Dar es salaam. Mamlaka nchini Tanzania kupitia Wizara ya Habari imekanusha kuwashikilia aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbrod Slaa na wenzake wawili (Wakili Mwambukuzi, na Mwanachama wa Chadema Mdude Nyangali).

Mr Kidevu (@KidevuMr) / Twitter

kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye imesema hakuna mtu aliyekamatwa kwa kukosoa mkataba wa bandari au atakayekamatwa kwa kukosoa mkataba huo na kuwa taarifa kwamba aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dk Wilbrod Slaa na wenzake wawili wamekamatwa kwa kukosoa mkataba huo si la kweli. " kuhusisha ukamatwaji wao na suala la Bandari ni upotoshaji'.

‘Hakuna aliyekamatwa nchini Tanzania, au atakamatwa kwa sababu tu ya kukosoa mkataba wa bandari au mradi wowote wa Serikali, mpango, au sera’, ilisema Sehemu ya taarifa hiyo.

Nape Nnauye Waziri mpya wa Habari – Bongo5.com

Wiki hiii Mashirika yanayotetea haki za binadamu ya ndani na nje likiwemo la Amnest International yametoa kauli kutaka Mamlaka nchini humo kuwaachia bila masharti, Dk. Slaa ambaye amewahi kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, mwanaharakati wa upinzani Mpaluka Nyagali na wakili Boniface Mwabukusi.

Watu hao waliokamatwa hivi karibuni, wengi wakihusisha na misimamo yao mikali kupinga mkataba wa ukuzaji na usimamizi wa bandari uliotiwa saini kati ya serikali ya Tanzania kampuni ya kimataifa ya uchukuzi ya DP World ya Dubai.

"Ukandamizaji wa mamlaka ya Tanzania dhidi ya wakosoaji wa mpango wa bandari unaonesha kuongezeka kwa kutouvumilia kwao upinzani. Mamlaka lazima ziache kuwashikilia wanaharakati kiholela kwa sababu tu ya kutoa maoni yao kwa amani na kuwaachilia mara moja na bila masharti wanaharakati hawa ili kuhakikisha kuheshimiwa kwa haki ya uhuru wa kujieleza,” alisema Tigere Chagutah, Mkurugenzi wa Amnesty International Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini.

Siku moja baada ya kauli hiyo, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) pamoja na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), walitoa kauli ya pamoja, mbali na kutaka waachiwe bila masharti, wamelitaka jeshi la Polisi kuheshimu sheria na haki za watuhumiwa pamoja na haki za binadamu nchini humo.

Akisoma taarifa hiyo ya pamoja ya wadau hao, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga alisema "Tunaamini kukamatwa kwao kuna uhusiano wa moja kwa moja na misimamo yao juu ya mkataba kati ya Tanzania na Emirate ya Dubai".

Hata hivyo kauli ya Serikali ya Tanzania inapinga hilo, ambapo watu hao wamekamatwa kwa makosa tofauti.

‘Watu hao watatu wamekamatwa na polisi baada ya kutoa vitisho mahsusi vya usalama ambavyo ni vya kihalifu. Vitisho hivyo vinajumuisha kutishia kuipindua serikali iliyopo madarakani serikali’, ilisema Taarifa ya Nape.

Tangu kusainiwa na baadae kuridhiwa na bunge , Mkataba huo wa bandari umeibua mjadala mkubwa nchini Tanzania, wapo wanaoamini hauna maslahi kwa nchi, jambo linalopingwa na Serikali. Mmoja wa waliokamatwa, Wakili Mwabukusi akiwa na wenzie walifungua kesi katika Mahakam Mbeya kupinga Mkataba huo, kesi ambayo hata hivyo Mahakama ilisema mkataba huo hauna shida.