- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI IMEPUNGUZA VIFO VYA MAMA KUTOKA 556 HADI 104 KWA VIZAZI HAI 100,000
DODOMA: Serikali imesema katika kipindi cha miaka minne imepunguza vifo vya mama na mtoto kutoka 556 kwa vizazi hai 100,000 hadi 104 kwa vizazi hai 100,000.
Hayo yamebainishwa leo Jumatatu Januari 20, 2025 na Waziri wa Afya Jenista Mhagama alipoambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) DKt. Tedros Ghebreyesus kukagua huduma za afya ya mama na mtoto (CEMOC) katika Kituo cha Afya Makole Mkoani Dodoma.
Waziri Mhagama amesema huduma za msingi ambazo zinatolewa katika kituo hicho ni pamoja na huduma ya uzazi mama na mtoto ili kuendelea kuokoa vifo vya mama na mtoto .
Aidha, amesema "Tumekuja hapa katika Kituo cha Afya Makole na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tedros Ghebreyesus kwa lengo la kuona juhudi za Serikali za kuhakikisha tunaokoa vifo vya mama na mtoto lakini pia miradi ambayo Serikali inaendelea kuisimamia,".