Home | Terms & Conditions | Help

January 22, 2025, 8:37 am

NEWS: WATUHUMIWA MAUAJI MTOTO GRAYSON MAHAKAMANI KWA MARA YA PILI

DODOMA: Washtakiwa wa mauaji ya mtoto Grayson Kanyenye wamefikishwa tena Mahakamani ikiwa ni mara ya pili, wakikabiliwa na shtaka la kumuua kwa maksudi mtoto huyo siku ya tarehe 25 Desemba, 2024.

Washtakiwa hao wawili ambao ni Tumaini Msangi anayetajwa kuwa ni mfanyakazi wa Airport na Kelvin Gilbert (Dereva Bodaboda) wote wakazi wa Ipagala Jijini Dodoma

Ikumbukwe kuwa watuhumiwa hao walifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza siku ya tarehe 30 Desemba, 2024 chini ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Denis Mpelembwa ambapo hawakutakiwa kujibu chochote.