Home | Terms & Conditions | Help

March 15, 2025, 10:45 am

NEWS: TANTRED YAFANIKIWA KUPANUA MASOKO KIMATAIFA

DODOMA: Katika kipindi cha mwaka 2023/2034/2025 , Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imefanikiwa kupanua masoko, kusaidia biashara za Tanzania kupata fursa za kimataifa, kujenga uwezo wa wafanyabiashara wadogo na wa kati, na kuboresha mifumo ya upatikanaji wa taarifa za biashara.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE), Latifa M. Khamis, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 13, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - Maelezo, jijini Dodoma.

Amesema kuratibu na kusimamia Mifumo ya Soko la Ndani kwa Uratibu wa DITF ambao ulipelekea mafanikio yafuatayo kwa kipindi cha mwaka 2020/21 -2023/24 Washiriki wa ndani wameongezeka kutoka 2,926 hadi 3,503, huku washiriki wa nje wakiongezeka kutoka 76 hadi 451.

"Nchi zinazoshiriki zimeongezeka kutoka 17 hadi 28,Watembeleaji wa maonesho wamefikia zaidi ya 300,701 ,Ajira za muda mfupi zimeongezeka kutoka 11,200 hadi 11,869,Mauzo ya papo kwa papo yamefikia shilingi bilioni 3.62," Amesema.

Na kuongeza "Fursa za mauzo kupitia maonesho zimefikia thamani ya shilingi bilioni 25.16,Mikataba ya kibiashara yenye thamani ya shilingi bilioni 176 ilisainiwa, ongezeko kubwa kutoka shilingi bilioni 5.6

Katika kipindi cha miaka minne mafanikio yafuatayo yalipatikana kupitia Kliniki za biashara;

Amesema Jumla ya wafanyabiashara 3,256 walihudumiwa kupitia kliniki zilizofanyika katika maonesho na mikutano ya kibiashara huku changamoto 1,324 ziliwasilishwa, ambapo 1,298 zilitatuliwa, na 26 zipo katika hatua za utekelezaji, hususan zinazohusiana na mitaji na vibali vya biashara.

Amesema katika kliniki hiyo Kampuni 482 zilipatiwa msaada wa usajili kupitia taasisi wezeshi kama BRELA, BPRA, na TRA, na biashara mpya zilianzishwa.

"Kampuni 137 zilisaidiwa kupata ushauri alama za ubora, vifungashio vinavyokidhi viwango vya soko la kimataifa, na mbinu za kuongeza thamani ya bidhaa, " Amesema

Na kuongeza "Wafanyabiashara 238 waliunganishwa na wanunuzi wa ndani na nje ya nchi kupitia mikutano ya B2B na B2G, ambapo biashara za bidhaa kama asali, mazao ya nafaka, mbogamboga, na viungo zilifanikishwa, " Amesema.

Aidha ameeleza Wafanyabiashara 312 walipatiwa mafunzo kuhusu mbinu bora za biashara, taratibu za forodha, na miongozo ya kodi kupitia TRA.