- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: WAKULIMA KUJADILI MCHAKATO WA BAJETI.
DODOMA: Serikali imelalamikiwa kwamba haiweki wazi mchakato mzima wa bajeti hasa kwa wananchi waishio vijijini na badala yake wanashuhudia miradi ya maendeleo ikiendelea kutekelezwa bila ushirikishwaji.
Kauli hizo imetolewa na wakulima wa Wilaya za Chamwino (Dodoma) na Halmashauri ya Singida walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo yameandaliwa na Shirika la Action Aid kupitia mradi wa Trasnformative Impact Fund (TIF) ili kuwapa mbinu za kuhoji miradi na mwanzo wa bajeti.
Akizungumza kuhusu mpango huo, Mkulima Sendeu Mjelwa kutoka kijiji cha Msanga wilaya ya Chamwino amesema hakuna bajeti shirikishi zinazoanzia ngazi ya chini vijijini badala yake yanapelekwa maagizo kutoka ngazi ya juu na ndiyo maana utekelezaji wake umekuwa na changamoto hasa miradi mikubwa inayojengwa.
Sendeu amesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wa vijijini hasa wakulima wakihoji namna gani wanashushiwa bajeti kutoka mamlaka za juu bila ya kujua nani aliamua kujenga mradi au kutoa kiasi cha fedha kwa ajili ya kitu chochote kwenye kijiji ikiwa hakuna ushirikishwaji.
“Hasa sisi vijana tumekuwa wahanga kwenye mambo haya na tunashindwa wa kumhoji, huko vijiji viongozi hawana majibu ni lini na namna gani mchakato wa bajeti huwa unafanyika badala yake tunaona miradi mikubwa inajengwa wakati mwingine hata ile ambayo si kipaumbele chetu,” anasema Sendeu.
Kwa upande wake Agripina Ndahani amesema tatizo kubwa linalowaumiza wananchi ni uelewa hasi kuhusu masuala ya bajeti kwani wengi wanaamini chombo pekee kinachopanga bajeti ni Serikali kuu na kwamba ndiye msimamizi.
Agripina amependekeza Serikali kutumia muda mwingi katika kutoa elimu kuhuhu bajeti ya serikali na jinsi inavyoanza mchakato wake akisistiza Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wawe wa kwanza kuipokea elimu hiyo.
Hata hivyo ofisa Kilimo na Mifugo kutoka Halmashauri ya Singida Adam Sungita amesema ushiriki wa wananchi katika bajeti ni mkubwa na mara nyingi huanzia ngazi ya chini kwa wananchi wenyewe.
Sungita amesema ushiriki wa kuandaa bajeti siyo lazima ujikite kwenye pesa bali wananchi wanaweza kukaa na kuibua mradi au shughuli nyingine.
Ofisa huyo amesema mara nyingi watu wanalalamika mapato ya vijiji vyao hayajulikana kwenye matumzi kwa madai yanachukuliwa na Halmashauri, lakini wanasahau kuwa kijiji kinaweza kuwa na uwezo wa kukusanya labla Sh14 milioni wakati kijiji kingine wakaweza kukusanya hadi Sh200 milioni kwa hiyo zinapaswa kuwekwa katika mfuko mmoja ndipo zifanyiwe mgao katika maendeleo.
Mwisho,……..