- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI UMMY: TUMEFANIKIWA KUDHIBITI UGONGWA WA CORONA
SERIKALI imesema kuwa imefanikiwa kudhibiti na kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya virusi vya corona nchini huku ikiwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ili kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 8, 2020 na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwenye ziara yake ya kushtukiza kwenye Kituo cha Afya cha Ngamiani Tanga ambapo alizungumza na wahudumu wa Afya na kupokea msaada wa vifaa vya kudhibiti Ugonjwa wa COVID19 vilivyotolewa na Shirika la Water Mission Tanzania.
Mwalimu alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na wananchi wake na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa imeweza kuudhibiti ugonjwa huo huku ikiendelea na juhudi za kuumaliza kabisa.
“Kwa kiasi kikubwa tumeweza kuidhibiti corona na sasa tunaelekea kuumaliza kabisa, tuachane na kusikiliza baadhi ya vyombo vya habari vya wenzetu wanaotaka kututisha kuhusu ugonjwa huu"- Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
"Lakini pia ndugu zangu waandishi wa habari mnaona hali halisi hapa tumefika hakuna mgonjwa hata mmoja wa corona, hivyo muwajulishe wananchi habari hizi kwamba ugonjwa tumeudhibiti na hatuna kituo chenye wagonjwa wa corona ndani ya mkoa wetu" Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
Aidha alifafanua kwamba wananchi wote wanaokwenda kupata huduma za kijamii ni lazima waendelee kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya corona kwa kufuata maagizo ya serikali na wataalamu wa afya.