- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI MAKAMBA AKANUSHA KUPANDA KWA BEI YA UMEME
Dodoma. Waziri wa Nishati nchini Tanzania January Makamba amekanusha vikali taarifa ya kupanda kwa bei ya umeme nchini na kuwataka wananchi kupuuza taarifa hizo.
Makamba amesema kuwa kupanda kwa bei ya umeme kunamchakato mrefu kwasababu kunahusisha maoni ya watu na wadau lazima washirikishwe katika mchakato huo.
Kauli hiyo ya Serekali imetololewa leo Ijumaa Juni 10, 2022 wakati Waziri wa Makamba akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Nyasa (CCM), Stella Manyanya.
Mbunge huyo alihoji kama ni kweli bei ya umeme imepanda maana katika mitandao ya kijamii kuana taariza inazunguka kuwa bei ya umeme imepanda.
Akijibu swali hilo, Makamba amesema si kweli kwamba bei ya umeme imepanda na kuwa Serikali inasikitishwa na uvumi huo.
Amesema kuwa tayari wameshazitaka mamlaka zichukue hatua kwa watu ambao wanaeneza uvumi huo.
“Mchakato wa kupandisha bei za umeme ni mrefu na unahusisha maoni na wadau ni lazima washirikishwe pale bei inapotaka kupandishwa,”amesema Makamba.
Amesema mchakato huo sio wasiri ni lazima uwashirikishe wadau watoe maoni yao.
Naye Mbunge wa Viti Maalum, Salome Makamba alihoji Serikali inampango gani wa kuhakikisha kuwa maeneo ya viwanda katika jimbo la Shinyanga mjini yanapata umeme.
Akijibu swali hilo Makamba amesema Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limeanzisha programu kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwemo kwenye viwanda na migodi.