- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI MAJALIWA: TAKUKURU HAKIKISHA WANACHI HAWARUBUNIWI KWENYE UCHAGUZI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha Watanzania hawarubuniwi na wagombea wa nafasi mbali mbali katika uchaguzi mkuu ujao ili watumie vizuri utashi wao wa kisiasa kuchagua viongozi bora.
“Sote tunatambua kuwa Oktoba, mwaka huu Taifa letu litaendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani… mna jukumu zito la kuhakikisha Watanzania hawarubuniwi na msimuonee au kumpendelea yeyote kwa maslahi yenu binafsi.”
Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Agosti 12, 2020) alipofungua jengo la Intelijensia TAKUKURU Makao Makuu Dodoma. Amewasihi watumie vizuri ofisi hiyo kukusanya taarifa muhimu za kiintelijensia zinazowahusu wagombea, vyama au wananchi watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi mkuu.
Waziri Mkuu amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 28, 2020 na kwamba wanawajibu wa kuchagua Serikali bora na kiongozi bora atakayewaletea maendelea maendeleo. “Chagueni kiongozi mwenye maono aliyetenda na atakayetenda.”
“Tayari tumeshuhudia mking’ata baadhi ya wagombea waliojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye hatua za awali za uteuzi wa wagombea kupitia vyama vyao. Msiache; endeleeni kukaza uzi na kuwadhibiti wote wenye kujihusisha na vitendo hivyo,” amesisitiza.
“Niungane pia na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kuwasihi wanasiasa na wagombea wenzangu wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu tuache kutumia rushwa kwa lengo la kununua uongozi.”
Waziri Mkuu amesema wanapoelekea kwenye uchaguzi mkuu, ni vema Watanzania wote na viongozi wakazingatia nasaha za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, katika moja ya hotuba zake alipowataka wajiulize kwamba mgombea anayetumia rushwa kununua kura amepata wapi fedha hizo na je, akipata uongozi, fedha hizo atazirudishaje.
Amesema: “Kwa hivyo, nasi ifike mahala tuwahoji hawa wanaotutia doa. Je, wewe mwenzetu unayetumia rushwa kununua uongozi umepata wapi fedha hizo? Na je? tukikuchagua, utarejesha vipi fedha hizo? Nitoe wito kwa Watanzania wote, msikubali kuwachagua wagombea wanaotumia rushwa ili kupata nafasi za uongozi.”