- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI MAJALIWA: SEREKALI INAWAPENDA WANANCHI WAKE
Tanga. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali inawapenda wananchi wake na inaendelea kufuatilia kwa karibu magonjwa yote nchini, lakini wananchi waendelee kuchukua tahadhari ikiwemo kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa.
Kauli ya Waziri Majaliwa ameitoa hii leo Feb 20, 2021 wakati akitoa Salama za pole kutoka Serekalini kwenye mazishi ya Aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi.
Majaliwa amesema Kuhusu ugonjwa wa corona inafahamika kwamba hii ni vita na imeanzia kwa wakubwa na bado inaendelea, hivyo ni vyema wananchi wakajiridhisha na vitu wanavyotumia ikiwemo barakoa, kama ambavyo Rais Magufuli amewahi kutahadharisha.
Amewashukuru waumini viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea Taifa kama ambavyo Rais Dkt. Magufuli alihimiza jana, na kwamba jana Waislamu walitimza, leo Wasabato na kesho anaamini wengine wataendelea.