Kauli ya Majaliwa ameitoa jana Desemba 31, 2021 jimboni kwake Ruangwa mkoani Lindi, wakati akiwa kwenye mapumziko yake ya mwisho wa mwaka, na kusema kwamba serikali za awamu zote zimeendelea kuheshimu uwepo wa dini nchini kwani miongozo na mafundisho yanayotolewa na viongozi wa dini mbalimbali yanawafanya waumini wao kuwa raia wema.
"Nchi hii imeshikwa na Mwenyezi Mungu na ni kwa sababu viongozi wa dini wanaendelea kuliombea Taifa hili, kwahiyo na sisi tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba nchi hii inabaki kwa salama," amesema Waziri Mkuu.
Majaliwa amewataka Watanzania wampe nafasi Rais Samia ya kufanya kazi kwa sababu amekuwa serikalini kwa muda mrefu na anajua ni nini Watanzania wanatamani serikali yao iwafanyie na kusema madaraka yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu na yeye ndiye hupanga nani awe nani na kwa wakati gani.
“Kila nafasi imetengenezwa na Mwenyezi Mungu na kila anayekwenda kuongoza Mwenyezi ndiye amesema wewe utakuwa pale, na kama hajasema, hutokuwa, utatumia hela nyingi na zitapotea bure, utakwenda na mambo mengine ya giza, lakini hutomudu, Mungu keshasema huyu ni huyu, tuwaheshimu walioko kwenye nafasi za kuwatumikia Watanzania wafanye kazi zao kwa weledi,”ameongeza.
NINI MAONI YA MWANDISHI
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu Majaliwa inatoa nafasi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kusema kuwa ndani ya Serekali ya Rais Samia mambo sio shwari inaonekana wapo baadhi ya viongozi wanatamani kushika au kupata nafasi aliyonayo Rais Samia kwasasa na kuona kwamba Mama hastaili kuwa katika kiti kile.
Katika hilo Ndani ya Chama chao cha CCM kumetokea viongozi mbalimbali na wanachama wa chama hicho wamejitokeza kutoa kauli za kumuunga mkono Mwenyekiti wa chama chao ambaye pia ndio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassani ya kusema kuwa wanamuunga mkono kwenye jambo lolote analofanya rais huyo.
Kauli ya viongozi hao ya kumuunga mkono Rais Samia imekuja siku chache mara baada ya kauli ya Spika wa Mbunge la Tanzania Job Ndugai kupishana na kauli Rias Samia juu ya Msimamo wa Serekali kukuopa fedha katika mambo ya kimaendeleo.
Spika Ndugai mnamo Desemba 28 mwaka huu alisema kuwa ni vyema kama nchi iachane na maswala ya kukopa kopa fedha kwani inazidi kuongeza idadi ya deni la taifa huku akibainisha kuwa mpaka sasa Deni la taiafa limefika trilioni 70.
Spika ndugai alishauri ni vyema kama nchi tukaendelea kutafuta pesa kupitia tozo za miamala ya Simu, kauli hiyo ya Spika ilipingwa vikali siku inayofuata na Mkuu wa nchi Rais Samia na kusema kuwa kama nchi nilazima wakope kwenye miradi mikubwa mikubwa ili kuweza kumaliza haraka badala ya kutegemea tozo.
Baada ya kauli ya viongozi hao kumetokea hisia mseto kutoka kwa wadau wa Siasa, wananchi na wanasiasa kuuliza inakuaje mihimili miwili hii inapishana kauli ikiwa wote wanaendeshwa na ilani moja ya chama chao.