- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI MAJALIWA: IDADI YA WAGONJWA WA CORONA YAPUNGUA NCHINI
Dodoma. WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amesema idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona nchini imepungua na kuwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huo.
Akiongea Jana Mei 24, 2020 katika ibada ya Eid UL Fitr iliyofanyika katika Msikiti wa Gadaffi Jijini Dodoma amesema Jiji la Dar es Salaam katika Hospitali ya Amana kulikuwa kuna wagonjwa 12,lakini kwa taarifa ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Dk. Rashid Mfaume amebaki mgonjwa mmoja, Mloganzila walikuwa 6 kwa sasa amebaki mmoja, huku Temeke kukiwa hakuna mgonjwa hata mmoja.
Alisema kwa Mkoa wa Dodoma kulikuwa na wagonjwa 12, sasa wamebaki watatu, huku Pwani kukiwa na wagonjwa watatu kati ya 22,kwa upande wa Hospitali binafsi Aga Khan ilikuwa na wagonjwa 11, sasa wamebaki wanne na katika Hospitali ya Palestina kulikuwa kuna wagonjwa 14,sasa hakuna hata mmoja.
Ibada hiyo iliongozwa na Sheikhe wa Mkoa wa Dodoma,Mustapha Rajabu,ambapo Majaliwa alisema jana asubuhi alizungumza na Dk. Mfaume na kumweleza wagonjwa wamepungua.
“Tunaposema ugonjwa umepungua ni kweli, taarifa za leo (jana) saa 1.30 asubuhi kwa wagonjwa wetu waliothibitishwa Mkoa wa Dar es salaam ambao ulikuwa na maambukizi mengi tukadhani tuchue Hospitali yote ya Amana na tulikuwa tumeandaa eneo la Sabasaba huko wakijaa tuwapeleke huko.
“Pale Temeke tukaomba wodi moja ya vitanda 10 kwa ajili ya kulaza wagonjwa, tukaacha Muhimbili na Mloganzila kubwa kwa sababu ya wagonjwa wengine.
“Tarehe 17,rais alituambia wamebaki wagonjwa 12, ninafurahi kuwaambia nimezungumza na Daktari wa Mkoa wa Dar es salaam asubuhi ya leo (jana) amebaki mgonjwa mmoja.
“Mloganzila pale tumejenga kambi yenye vitanda 30 na taarifa ya rais kulikuwa kuna wagonjwa 6 kwa taarifa ya Mganga Mkuu wa Dar es Salaam amebaki mgonjwa mmoja.
“Hospitali ya Temeke rais alisema hakuna mgonjwa na leo napenda niwaambie hakuna mgonjwa na mnajua Temeke,Mbagala Gongolamboto Tandala jinsi kulivyo na watu wengi, tunashuku ‘allah’ kwa kutokuwa na mgonjwa,”alisema.
Alisema wagonjwa wachache bado wapo katika Hospitali za binafsi ambapo alidai Aga Khan taarifa ya Rais ilisema kuna wagonjwa 11 lakini kwa sasa ambao wapo katika uangalizi ni wanne pekee huku,Hospitali ya Palestina kukiwa hakuna mgonjwa ambapo awali kulikuwa kuna wagonjwa 14.
“Lakini tuna hospitali za binafsi ambazo zimeunga mkono jitihada za Serikali kwa kutenga maeneo ya wagonjwa kama vile Hospitali ya Kairuki ilikuwa na wagonjwa wanne leo hakuna mgonjwa aliyethibitishwa.
“Palestina, rais alisema kuna wagonjwa 14 kwa sasa hakuna mgonjwa hata mmoja.Regence hakuna mgonjwa na Temeke pia.
“Wagonjwa bado tunao katika Hospitali ya Aga Khan tarehe 17 mheshimiwa Rais alituambia wapo 11 lakini wanne ndio wanaangaliwa kwa karibu,”alisema.
Alisema Mkoani Pwani katika Hospitali ya Kibaha kulikuwa kuna wagonjwa 22 lakini kwa sasa waliobaki ni watatu pekee huku kwa Mkoa wa Dodoma kukiwa na wagonjwa watatu kati ya wagonjwa 12 waliokuwa katika kituo cha Mkonze.
“Kule Kibaha walikuwa 22 leo kati ya hawo watatu ndio wanaangaliwa kwa karibu.Hapa kwetu Dodoma Mkonze 12 jana (juzi) tulikuwa na wagonjwa watatu hata asubuhi hii tumeamka na wagonjwa watatu hawa wote wanaangaliwa naamini Mwenyezingumu taendelea kutusaidia,”alisema