- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WAZIRI ATAKA WASANII WAKONGWE KUTEULIWA KUONGOZA SANAA
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wa BASATA na COSOTA kuteua viongozi wenye fani ya sanaa hasa wakongwe wanaoijua sanaa vizuri ili waende kusimamia maswala ya biashara zao na kulinda haki zao dhidi ya walanguzi.
"Tusijifungie maofisini, twende tukawatafute,
"kwenye nafasi tuweke watu wenye fani ya sanaa, wasanii wakongwe wapo wanaijua sanaa, tuwateue kwenye nafasi mbalimbali hasa za BASATA ili wakasimamie biashara zao, wakasimamie kutafuta wateja, kuangalia walanguzi na haki zao za msingi.
“Mnaponiletea mapendekezo kwenye mabodi, nileteeni majina ya wasanii, kwa mfano Kenya wanaosimamia ni wasanii wenyewe akina Juakali, na sisi tufanye hivyo ili wakalinde haki zao wenyewe ili kuiendeleza tasnia, hawatakubali sanaa ianguke kwani watakuwa wameanguka wao,” amesema Mchengerwa.
Aidha Waziri Mchengerwa amewataka viongozi wa BASATA na COSOTA kuhakikisha wasanii wote wanasajiliwa hususani wale wakubwa ambao mpaka sasa hawajasajiliwa kwani hakuna msanii mkubwa kuliko nchi.
“Nitoe maelekezo kwa COSOTA na BASATA, hatutegemei kusikia wasanii wamesajiliwa wachache, sitegemei kusikia msanii mkubwa hajasajiliwa, tutaanza kuhoji uwezo wa tuliowapa dhamana.
“Jukumu letu sisi serikali ni kuwaunganisha wasanii wote, hakuna msanii mkubwa kuliko nchi, sisi tuliopewa mamlaka twende tuwanyenyekee, wanatoa mchango kwa nchi inanufaika na kupitia kodi.