Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:16 pm

WAZIRI AAGIZA KUFANYIKA UCHUNGUZI KUBAINI MADUDU HOSPITALI YA MWANANYAMALA

Waziri wa Afya Doroth Gwajima ameagiza kufanyika kwa uchunguzi kubaini tuhuma zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii juu ya watoa huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala jijini Dar es salaaam kutohudumia wagonjwa ipasavyo.

Waziri ameyaelekeza Mabaraza ya kitaaluma yafike katika hospitali hiyo na kufanya ufuatiliaji ili kubaini ukweli wa taarifa hizo kisha kuchukua hatua stahiki.

Aidha Wizara ya afya imesema taarifa hiyo ya uchunguzi iwasilishwe Wizara ya Afya Dodoma, tarehe 02 Januari,2022, saa saba kamili mchana.