- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
WATUMISHI 3 WA CHADEMA WAKAMATWA KWA KUCHOMA OFISI ZA CHADEMA ARUSHA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linawashikilia watumishi watatu wa chama cha Upinzani CHADEMA kwa tuhuma za kuhusika moja kwa moja na tukio la kuchomwa moto kwa ofisi za chama hicho Kanda ya Kaskazini, zilizoteketea Agosti 14, 2020, na kusababisha uharibifu wa mali wa thamani ya zaidi ya Milioni 5 baada ya tathmini kufanyika.
Taarifa hiyo imetolewa hii leo Septemba 3, 2020, na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Salum Hamduni.
ACP Hamduni amesema kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea, uchunguzi wa kina ulifanyika kuwabaini na kuwakatama watu wote waliohusika katika tukio hilo ambapo Agosti 19 alikamatwa mlinzi wa Ofisi hiyo aitwaye Deogratius Malya.
Mbali na huyo Jeshi hilo pia limemkamata Leonard Cathbert Ntukula, ambaye ni Dereva wa CHADEMA na Mkazi wa Tabata Jijini Dar es Salaam, pamoja na Prosper Masatu Makonya, ambaye ni Afisa mhamasishaji wa CHADEMA Makao Makuu na Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam, ambao wote hao walikamatwa kati ya Agosti 28 na 29 mwaka huu.
Aidha Kamanda Hamduni ameongeza kuwa, baada ya kukamilisha upelelezi, jalada la kesi hiyo limepelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kulisoma na kulitolea maamuzi ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuandaa hati ya mashtaka, na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.