Home | Terms & Conditions | Help

April 4, 2025, 7:37 am

WATETEZI KENYA WAITAKA SEREKALI KUJENGA MASHULENI VYUMBA VYA KUNYONYESHEA

Nairobi. Muungano wa kutetea haki za walimu wanawake nchini Kenya (Kewota) umeitaka Serekali kupitia wizara ya elimu kuanzishaa vituo vya kunyonyeshea watoto shuleni ili kuhakikisha walimu wote wanaojifungua wapo karibu na watoto wao wachanga katika hatua zao za mwanzo wa malezi.

Muungano huo unasema kwamba sheria ilipitishwa 2016 ikiitaka serikali kujenga vituo hivyo katika taasisi zote za umma lakini shule za umma bado hazijazingatia sheria hiyo.

Mkurugenzi wa Kewota, Benta Opande, alisema walimu wa kike hasa walio na watoto wachanga hulazimika kwenda nyumbani mara kwa mara shule zinapofunguliwa ili kunyonyesha na hivyo kupoteza wakati na pesa.

“Tunataka kusaidia walimu wanawake walio na watoto wachanga na wanaohisi haja ya kwenda nyumbani kuwanyonyesha,” alisisitiza Bi Opande.