Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:13 am

WAKALA WA PAUL POGBA: SASA INATOSHA POGBA KUICHEZEA MAN UNITED

Wakala wa Kiungo staa wa club ya Manchester United Paul Pogba Bw. Mino Raiola ameiambia Tuttosport kuwa kwasasa imefika mwisho kwa mteja wake kuendelea kuitumikia club hiyo ya Manchester.

"Ninachoweza kusema kwasasa kuhusu Paul Pogba nikwamba imetosha sasa yeye kubaki Manchester United" amesema Raiola

Manchester United na Pogba mpaka sasa wemeshindwa kukaa meza moja kujadili namna ya kuongeza mkataba wake unaoishia mwaka 2022.

Pagba mwenye umri wa miaka 27 amekuwa na wakati mgumu kwa sasa na club yake, hasa kutokana na presha ya mashabiki wa club hiyo.

Kiungo huyo wa Ufaransa mara nyingi amekuwa akionesha niya yake ya kutaka kujiunga na club ya Real Madrid au club yake ya zamani ya Juventus kabla ya kuingia msimu wa Corona