Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 8:17 pm

URUSI: MAZUNGUMZO YOYOTE HAYATASIMAMISHA OPERESHENI

Moscow. Serikali ya Urusi imeionya vikali Ukraine kwamba operesheni za kijeshi zinazoendelea nchini humo, hazitasimamishwa katika mazungumzo yoyote yanayowezekana kufanyika.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi, Interfax.

Serekali ya Moscow ilisema ujumbe wake uko tayari kukutana na serikali ya Ukraine katika mji wa Gomel nchini Belarus, eneo ambalo limekataliwa na Rais Volodymyr Zelenskiy akisema serikali ya Minsk yenyewe imehusika katika uvamizi wa Urusi.Hata hivyo, katika hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya mtandao amesema yupo tayari kwa mazungumzo na kutoa mapendekezo ya miji ya Warsaw, Bratislava, Budapest, Istanbul na Baku.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 44 amesema pia hata katika eneo lolote ambalo makombora yake hayawezi kurushwa litakuwa eneo zuri kwa mazungumzo na kwa namna hiyo mazungumzo yatakuwa ya kuaminika, na kumaliza vita.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, Alhamis iliyopita alianzisha mashambulizi kamili dhidi ya Ukraine ambayo hadi wakati huu yamegharimu maisha ya takribani watu 200 na kulaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa.