Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 2:20 pm

UCHAGUZI WA URAIS KENYA: RUTTO NA ODINGA WASHINDANA VIKALI

NAIROBI. Uchaguzi Mkuu nchini Kenya umekuwa na ushindani mkali, Zaidi ya vituo vya kupigia kura 43,000 vimewasilisha matokeo yao ya uchaguzi wa rais kutokana na kura zilizopigwa jana Jumanne.

Matokeo ya awali yanaonyesha ushindani mkali kati ya wagombea wawili wakuu wa uchaguzi wa urais, Naibu Rais William Ruto na Raila Odinga, kiongozi mkongwe wa upinzani ambaye sasa anaungwa mkono na chama tawala chini ya Uongozi wa Rais Kenyatta.

Mpaka kufikia Saa 08:35 Asubuhi, Mgombea wa UDA, Naibu Rais William Ruto bado anaongoza kwa kura 5,508,017 sawa na 49.68% huku Mgombea wa Azimio la Umoja, Raila Odinga akiwa na kura 5,426,725 sawa na 48.95%

Tume itatangaza matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa urais baada ya kuthibitisha fomu 46,229 zilizowasilishwa kutoka katika vituo vya kupiga kura kote nchini. Kuthibitishwa kwa matokeo haya kunaweza kuchukua siku kadhaa.

Wakati huo huo Tume ya uchaguzi inasema inaamini Wakenya milioni 13.2 wamepiga kura.

Tume hiyo ina hadi Agosti 16 kutangaza matokeo ya mwisho. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebnukati amewaomba Wakenya kuwa watulivu wakati shughuli ya kujumlisha kura ikiendelea.