- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
TUNDU LISSU: NCHI YETU IKO NJIA PANDA
Naibu Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tazanzania Tundu Lissu hii leo ametangaza rasmi nia ya kuwania kiti cha urais kupitia chama chake cha Chadema katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza kwa njia ya mitandao akiwa nchi za Magharibi, Lissu ametangaza nia ya kuwania urais nchini Tanzania, katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
''Sasa ninapenda kuwataarifu rasmi kwamba nimetangaza rasmi nia yangu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
"Tayari nimeshawasilisha taarifa rasmi ya kutangaza nia hiyo kwa katibu mkuu wa chama chetu kama iliyoelekezwa kwenye maelekezo yake kwa wanachama wa chama chetu.''
''Katika uongozi wangu, nitaondoa vikwanzo vyote vinavyokandamiza vyama vya siasa na nitalinda mfumo wa vyama vingi badala ya kukandamiza vyama vinavyopingana na serikali iliyopo madarakani'' - Tundu Lissu
"Nchi yetu ipo katika njia panda na Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakuwa na umuhimu mkubwa katika historia ya nchi yetu".
Katika hotuba yake iliyopeperushwa mubashara mchana huu kwa njia ya mitandao ya kijamii, Lissu ameahidi kuwa endapo atapata ridhaa ya kuiongoza Tanzania serikali yake haitalipiza kisasi.
Kwa siku kadhaa zilizopita, kumekuwa na fununu mitandaoni kuwa huenda Lissu akajitosa ulingoni kuwania urais kupitia Chadema, na hii leo amelithibitisha hilo.
Lissu mwenyewe aliwahi miaka ya nyuma kusema kuwa angelitamani siku moja kuwania urais wa Tanzania.
NINI LISSU ATAFANYA AKIWA RAIS
Lissu amekuwa moja ya wakosoaji wakuu wa serikali ya Rais John Pombe Magufuli kwa miaka mitano iliyopita. Hata kwenye hotuba yake ya leo pia ameendeleza ukosoaji wake kwa serikali.
''Nina wajibu wa kutaja kile kilichonisukuma kutaka kugombea nafasi hii ya juu kabisa kiungozi katika mfumo wa kikatiba wa nchi yetu yaani Rais wa Jamuhuri ya Muungano .Kwa kipindi cha miaka mitano itakayoishia Oktoba mwaka huu nchi yetu imetawaliwa na serikali ya Rais John Pombe Magufuli na Chama cha Mapinduzi , CCM kwa namna ambayo imeiweka nchi yetu katika mtihani mkubwa kiuchumi, kisiasa na kidiplomasia.
Kwa mtihani huu nchi yetu iko njia panda, na kwa vyovyote vile itakavyokuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na umuhimu mkubwa katika historia ya nchi yetu''.
Lissu ameituhumu serikali ya Rais Magufuli kwa kile alichokiita kuingilia mihimili mingine ya dola kama Bunge na Mahakama.
Endapo atapitishwa na chama chake na kushinda urais kwenye uchaguzi wa Oktoba Lissu ameahidi kuendesha serikali yake kwa misingi ya katiba na kuheshimu uhuru wa mihimili mingine.