- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
TANZIA: WAZIRI WAZAMANI BASILI MRAMBA AFARIKI DUNIA
Waziri wa zamani wa fedha na mipango nchini Tanzania, Basil Pesambili Mramba (81) , amefariki dunia hii leo Jumanne Agosti 17, 2021, katika Hospitali ya Regency, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa ya kifo cha Mramba kimetolewa na ndugu wa marehemu, Godfrey Mramba.
July 6, 2015 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela Mramba pamoja na Mwenzake aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili.
Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa kudhibiti madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart (ASSAYERS) Government Business Corporation waliingia mkataba na kampuni tanzu kukagua uzalishaji wa madini ya dhahabu, kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.