- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: YANGA NA TFF WAMALIZA UTATA
Dar es salaam. Mgogoro uliokuwepo unafukuta kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu ya wanajangwani ya Yanga Africa umefikia kikomo baada ya Serikali kuzikutanisha pande zote mbili na kila mmoja kutoa dukuduku lake na kufikia muafaka.
Kikao hicho kimeitishwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuongozwa na katibu mkuu wake, Dk Hassan Abbas lengo likiwa kumaliza tofauti juu ya pande hizo mbili katika masuala mbalimbali ambayo yalikuwa hayaendi sawa na kuleta sintofahamu ambayo ilikuwa inaharibu taswira ya mpira nchini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa club ya Yanga, Mfikirwa amesema kikao hicho kimefanyika chini ya usimamizi wa Serikali na pande zote kufikia muafaka kwa faida ya soka la Tanzania:
“Nashukuru Serikali imetimiza ahadi yake ya kutukutanisha na uongozi wa TFF, na kueleza yale malalamiko yetu na pia nafurahi kuona muafaka umefikiwa kwa maslahi mapana ya mpira wa Tanzania, “alisema Mfikirwa.