Home | Terms & Conditions | Help

November 22, 2024, 7:44 pm

SPORTS: YANGA KULIPWA BILIONI 41 NA AZAM MEDIA

Dar es Salaam. Klabu ya Yanga imeingia mkataba wa maudhui na Azam Media wenye thamani ya Sh41 bilioni pamoja na kodi ya Ongezeko la Thamani yaani VAT. Mkataba huu utadumu kwa kipindi cha miaka 10.

Makubaliano ya Mkataba huo yamesainiwa leo Alhamisi Julai 8, 2021 jijini Dar es Salaam na mkurugenzi mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando na mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla.

Tafsiri ya Mkataba huo unamaanisha kuwa Yanga itapokea Sh200 milioni kwa mwezi kwa msimu ujao, fedha ambayo itakuwa ikiongezeka kila msimu.

Pia, mkataba unaeleza kwamba Azam Media itatoa bonasi ya Sh44.4 bilioni kwa miaka 10, endapo klabu hiyo itamaliza ligi ikiwa katika nafasi ya kwanza au ya pili katika kila msimu.