Home | Terms & Conditions | Help

April 5, 2025, 2:28 am

SPORTS: RAMOS AONDOLEWA KWENYE KIKOSI CHA HISPANIA

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Hispania, Luis Enrique leo amewasilisha Orodha ya wachezaji 24 watakao peperusha bendera ya timu ya taifa kwenye Mashindano ya Euro 2020,

ambapo habari kubwa ni kuacha kwa nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos 35 ambaye amecheza mechi 180 za timu yake ya taifa na ameitumikia Club yake kwa mafanikio makubwa.

Nahodha huyo wa Real Madrid bado kiafya hayuko katika hali nzuri, baada ya shida kadhaa za majeraha ambazo zimemrudisha nyuma msimu huu.

Gumzo kubwa pia ni kwamba Hispania itaenda kwenye Michuani ya Euro mwaka huu bila mchezaji hata mmoja wa Real Madrid, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia.

Hiki ndio kikosi kipya cha Hispania

Magolikipa: Unai Simon, David de Gea, Robert Sanchez;

Walinzi: Jose Gaya, Jordi Alba, Pau Torres, Aymeric Laporte, Eric Garcia, Diego Llorente, Cesar Azpilicueta, Marcos Llorente;

Viungo: Sergio Busquets, Rodri, Pedri, Thiago, Koke, Fabian;

Mafuadi: Dani Olmo, Mikel Oyarzabal, Alvaro Morata, Gerard Moreno, Ferran Torres, Adama Traore, Pablo Sarabia.