Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 5:32 pm

SPORTS: MORRISON ASHINDA KESI YAKE DHIDI YA YANGA

Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF chini ya kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji limesema kuwa mchezaji Bernad Morrison ameshinda kesi yake dhidi ya club ya Yanga.

Maamuzi hayo yametolewa jioni ya Leo Agosti 12, 2020 na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji Bw. Elias Mwanjala baada ya Kubaini kuwepo kwa mapungufu kadhaa katika mkataba huo baina ya Yanga na Morrison.

Kwa Maana hiyo Morrison ataendelea kuwa mchezaji halali wa wekundu wa msimbazi Simba.

“Ni mchezaji huru kutokana na mkataba wake kuwa na matatizo kidogo, mkataba uliokuwepo ulitakiwa kuisha tarehe 14 March, huku mkataba wa pili ulioletwa kwetu ukionyesha umesainiwa mwezi saba pia baadhi ya kursa kutokuwa na saini ya mchezaji na mtu mwingine kama shahidi kinachofuatiwa kwa sasa amepelekwa kwenye kamati ya maadili kwakua amesaini mkataba wakati akiwa na kesi” amesema Mwanjala.