Home | Terms & Conditions | Help

April 6, 2025, 7:15 am

SPORTS: MKUDE WA SIMBA NA MORRIS WAFUNGIA KUCHEZA NA TFF

Shirikisho la Soka nchini Tanzania Kupitia Kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo imemfungia kiungo wa Simba Jonas Mkude kucheza mechi 2 na faini juu ya shilingi laki 5, kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Biashara United.

Aidha Kamati hiyo imemfungia pia Mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison kucheza mechi mbili na faini ya shilingi laki 5, kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons.

Shirikisho hilo lemesema kuwa Utekelezaji wa adhabu zote hizo unaanza mara moja katika michezo ya leo.