- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: KIGOMA WADHIBITI UCHAWI MECHI YA SIMBA NA YANGA
Kigoma. Shirikisho la Mpira wa miguu mkoani kigoma(KFA) lemesema kuwa kwasasa Uwanja wa mpira wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma umekamilika kwa asilimia 90% kuelekea mechi ya fainali baina ya Simba Vs Yanga kwenye kombe la Azam Confideretion Cup Jul 25 mwaka huu.
Katibu wa Kamati wa Shirikisho hilo Omary Gindi amesema kwamba uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuingiza Mashabiki 17,000 watakaokaa na kusimama.
Katibu huyo pia ametoa wito kwa Mashabiki kutofika uwanjani hapo kwa aajili ya kuchukua nyasi na udongo kwaajili ya kufanya mambo ya jadi "Tulilikemea na kuna baadhi ya Watu walitaka kuchukua mchanga uwanjani tukawatimua, tumeweka ulinzi kuhakikisha mambo ya jadi hayana nafasi, na hakuna shabiki atakayeruhisiwa kuingia uwanjani bila sababu ya msingi" amessma Omary Gindi (KFA).
Katika hali ya Kumbukumbu Mkoa wa Kigoma unakwenda kuweka historia ya kipekee kabisa kwa Watani wa jadi yaani Simba na Yanga kucheza mchezo wao mkubwa zaidi kwa Tanzania na Afirka mashariki katika uwanja wa Lake Tanganyika tangu uwanja huo ujengwe.