- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SPORTS: KESI YA MORRISON NA YANGA YAFIKA TAMATI
Mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) leo imemaliza kulisikiliza kesi ya rufaa ya Klabu ya Yanga dhidi ya Mchezaji wa Simba Bernard Morrison.
Mara baada ya kumalizika kusikilizwa kwa kesi hiyo, CAS itatoa uamuzi kwa mujibu wa taratibu zake kuanzia sasa mpaka tarehe 24/08/2021.
Uongozi wa Yanga umewataka Wanachama, Wapenzi na Mashabiki kuwa na subira, wakati huu ambapo Mahakama hiyo inaendelea kukamilisha uamuzi wake.
Mwenyekiti wa club ya Yanga Dr. Msolla aliwahi kunukuliwa akisema wamelenga fidia kubwa dhidi ya Simba ili kukomesha masuala kama hayo kwenye soka.
Dk Msolla alisema suala la wao kushinda katika kesi hiyo ni la kawaida kutokana na jinsi sakata hilo lilivyoamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Taarifa kutoka yanga zinadai kuwa Uongozi wa Yanga wamepanga endapo watashinda kesi basi watani wao wajiandae kulipa kiasi cha sh milioni 600.