Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 6:55 pm

SPORTS: KARIM BENZEMA ASHINDA TUZO YA BALLON D’OR

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na club ya Real Madrid Karim Benzema ametangazw mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani ya "Ballon d'Or" kwa msimu wa mwaka 2021/2022.

Hafla ya tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani "Ballon d’or" imefanyika Jumatatu usiku katika ukumbi wa Theatre du Chatelet mjini Paris Ufaransa. Wachezaji 30 waliorodheshwa kuwania tuzo hiyo mwaka huu.

Ushindi huo unajiri baada ya kiwango chake kizuri kuisaidia Real Madrid kushinda Ligi ya Mabingwa na La Liga msimu uliopita. Benzema, ambaye ni mshindi wa kwanza wa Ufaransa wa tuzo ya kifahari zaidi ya mtu binafsi katika soka tangu Zinedine Zidane mwaka 1998, alifunga mabao 44 katika michezo 46 katika klabu yake ikiwa ni pamoja na 15 katika Ligi ya Mabingwa.

Benzema mwenye asili ya Afrika, amewapiku Sadio Mane wa Bayern Munich na Senegal, Kevin de Bruyne wa Manchester City na Ubelgiji na Robert Lewandowski wa Barcelona na Poland ambao wamekuwa wakiwania pia tuzo hiyo.