Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:38 pm

SPORTS: CAS KUTOA HUKUMU YA MORRISON OCTOBA 26 MWAKA HUU.

Mahakama ya Usuluhishi ya mchezo wa mpira wa miguu Duniani CAS wameahirisha kutoa uamuzi wa kesi baina ya club ya Yanga ya Jijini Dar es salaam na mchezaji wa Simba Bernard Morrison ambayo hukumu yake ilikusidiwa kutolewa leo Septemba 21 na badala yake sasa hukumu hiyo itatolewa Oktoba 26 mwaka huu.

Mmoja ya Mawakili anayewakilisha Yanga katika kesi hiyo Alex Mgongolwa amesema amepokea taarifa ya CAS leo ikieleza sasa hukumu hiyo imesogezwa mbele mpaka Oktoba 26.

“Siku zote ukiona kama hukumu inasogezwa mbele basi mleta shauri ana hoja ndio maana unaona hivyo, kwahiyo tunasubiri maamuzi hayo”-Alex Mgongolwa.