Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 1:12 am

SPIKA NDUGAI: UASKOFU WAKE NI HUKO HUKO SIO HAPA

Spika wa Bunge wa Tanzania Job Ndugai ameonesha kuchukizwa na kuchoshwa na vitendo anavyofanya Mbunge wa Kawe na Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwa kile alichodai kuwa anatumia nafasi yake ya Uaskofu Vibaya kupoteza Umma.

Kauli ya Spika ametoa mchana wa leo Mara baada ya kamati maalumu ya Bunge ya Maadili, Haki na kinga ya Mbunge kuwasilisha ripoti yake hii leo Agosti 31, 2021.

“Kuhusu Gwajima sisi hapa hatujamshitaki kama Askofu, tumemshtaki kama Mbunge Gwajima, habari za Uaskofu wake ni hukohuko, unaweza ukawa Askofu halafu kama wenzako hawaelewi Dini sio hivyo hayo ni macho ya Makengeza Watu ni Waumini sana”

“Mimi ni Mzee wa Kanisa la Anglikana wa miaka mingi, ni nafasi ya Mshauri wa Askofu, nimeshakwenda Nigeria kwa TB Joshua, nimeenda Makao Makuu ya Kanisa langu, Uyahudi nimekwenda mara nne, nimeenda kwenye Kijiji cha Yesu, Galilaya yote ile nilitembea naijua”

“Nimefika Nazareth, mara ya mwisho nimeenda na Mwalimu Mwakasege, tunatamba sisi?, sasa ukiwa Askofu utudanganye sisi?, Dini tunaijua, mnavyokwenda sio kutumia platform ya Dini kila Jumapili kuhamasisha “Mtusikilize, mtasikia mabomu kesho” Waziri wa Mambo ya Ndani uko hapa, Serikali mko hapa hii haiwezi kwenda hivi” — Spika Ndugai.