- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SEREKALI: VYETI FEKI HAWARUDISHWI KAZINI WALA HAWAPEWI MAFAO
Arusha. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amefafanua kwamba serikali haijawarejesha kazini wafanyakazi wote waliogushi vyeti na kuwalipa mafao yao wakati wakiwa watumishi.
Waziri Mchengerwa akizungumza na waandishi wa Habari jijini Arusha, amesema msimamo wa Serikali haujabadilika kuhusu watumishi hao walioghushi vyeti.
Aidha amesema kumekuwa na upotoshwaji kuhusu taarifa za watumishi hao jambo ambalo si sahihi.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kwamba serekali imedhamiria kuwarudisha kazini na kuwapa mafao yao wafanyakazi wote walioondolewa kazi mwaka 2018 kwa kadhia ya kughushi vyeti vyao vya taaluma.