- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SEREKALI: TENDO LA NDO SI HAKI YA MFUNGWA
Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Hamadi Masauni amesema haki ya tendo la ndoa kwa wafungwa hapa nchini siyo haki yao ya msingi.
Waziri Masauni ametoa kauli hiyo hii leo Jumanne Sept 13, 2022 Bungeni akijibu swali lilioulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Bahati Keneth.
"Tendo la ndoa ni haki lakini sio haki ya msingi, haki ya msingi ambayo tunatoa kwa wafungwa ni chakula, mavazi, malazi. Kuna mambo mengi ambayo yanapaswa kufanyika kwanza kabla ya kuruhusu haki hiyo gerezani "
“Serikali inaendelea kutoa haki mbalimbali kwa wafungwa...kwa mujibu wa sheria, haki ya faragha kwa wafungwa na wenza wao itaanza kutolewa pale ambapo mifumo ya kisheria, na miundombinu ya magereza itakapokidhi kutolewa kwa haki hiyo,"
- amesema Hamad Masauni.