- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SEREKALI: HAMZA ALIKUWA GAIDI WA KUJITOA MUHANGA
Mwanza. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), Camilius Wambura amesema kuwa Jeshi la Polisi nchini limekamilisha uchunguzi wa awali kuhusu tukio la kurushiana risasi baina ya Jeshi polisi na Kijana Hamza Mohammed na kudai kwamba uchunguzi huo umethibitisha mhusika wa tukio hilo Bw. Hamza alikuwa gaidi wa kujitoa muhanga.
Tukio hilo lililozusha taharuku mwezi uliopita lilisababisha kuuawa kwa watu wanne wakiwemo askari watatu wa Jeshi la Polisi na Mlinzi mmoja wa kampuini ya kibinafsi ya Ulinzi.
Mkurugenzi huyo wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai amewaeleza waandishi wa habari hii leo Septemba 2, 2021 jijini Mwanza kuwa mtuhumiwa alikuwa gaidi aliyedhamiria kuleta madhara makubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
DCI Wambura alikanusha mtuhumiwa kuwa alikuwa mmiliki wa migoni ya madini huko Chunya mkaoni Mbeya, kama ambavyo baadhi ya taarifa zilivyoripotiwa kwenye baadhi ya mitandao siku moja baada ya kuuawa.