- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
SEIF: TULIPISHANA UWAMUZI KUINGIA SEREKALI YA UMOJA WA KITAIFA
Dar es Salaam. Makamu mpya wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema uwamuzi wa chama chake cha ACT-Wazalendo kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) visiwani humo hakuwa mwepesi hata kidogo, kwani uliwapelekea baadhi ya wajumbe kupishana lakini mwisho wakaafikiana.
“Ulikuwa ni uamuzi uliotufikirisha sana, tumejadili na kupishana hatimaye tukifikia uamuzi. Moja ya sababu ilitufanya tukafikia uamuzi huu ni imani yako (Dk Hussein Mwinyi-Rais wa Zanzibar) na maneno yako binafsi, vitendo na ishara zako,” amesema Maalim Seif.
Kauli hiyo ya Maalim ameito hii leo Jumanne Desemba 8, 2020 muda mfupi mara baada ya kuapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar.
Kuhusu kupendekeza jina la Makamo wa Kwanza wa Rais.
“Walikataa(mimi kutokuwa makamo wa kwanza) kwa kuwa walisema mimi ni miongoni mwa watu waliongoza maridhiano na rais mstaafu Aman Abeid Karume mwaka 2009.Wameniambia kwa vile mimi nimelianza, basi nilimalize, waliniambia mimi ni mtu mzima na utu uzima ni dawa basi nimalizie. Wakanitaka nikubali ili nisaidie azma hii ya kutibu majeraha ya Zanzibar na kustawisha maridhiano.”
“Sikuweza kuwakatalia ndiyo maana leo nipo hapa nakula kiapo cha kuwa makamu wa kwanza wa rais,” amesema Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo.
Amefafanua kuwa SUK iliundwa kwa dhumuni kuwa chombo cha kusimamia, kuratibu na kuongoza juhudi za Wazanzibari katika umoja wa kitaifa, si chombo cha kugawana vyeo kwa kambi za kisiasa.
“Serikali ya umoja wa kitaifa ni sawa na chombo cha usafiri, ambacho msafiri yoyote awe wa meli, nchi kavu au angani. Lengo lake siyo kuingia katika meli, gari au ndege bali lengo ni kufika katika safari aliyoipanga.”
“Safari ya Wazanzibari ni maridhiano ya kweli mshikamano na kitaifa. Chombo chetu cha safari hiyo kwa wakati ni umoja wa kitaifa,” amesema.
Maalim Seif amesema ni wajibu viongozi wote waliopewa jukumu la kuongoza Serikali kuhakikisha suala hilo linatekelezwa ili chombo kifike.