- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RIPOTI: RIBA za bank nchini zaendelea kushuka
Dar es salaam: Wakopaji wa sekta mbalimbali za uchumi huenda wakapata unafuu kwenye mikopo kuanzia mwakani kutokana kuendelea kupungua kwa viwango vya riba ya mikopo baina ya benki.
Ripoti ya viwango vya riba za mikopo baina ya benki iliyoko kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania imeonyesha kwamba viwango vya mikopo baina ya benki vimeshuka hadi kufikia asilimia 10, kwa mujibu wa ripoti ya jana.
Kiwango hicho ni cha chini katika kipindi cha mwaka mmoja. Kuanzia Januari mpaka Desemba mwaka jana, viwango hivyo vilikuwa kati ya asilimia 9 na 17.
Hali ya kupanda kwa viwango vya riba baina ya benki mwaka jana na mwaka huu ilichangiwa na kupungua kwa ukwasi kwenye soko, hali iliyosababisha kupungua kwa amana za wateja pamoja na mikopo kwenye sekta za uchumi.
Sekta zilizokumbwa na upunguaji wa mikopo mwaka jana na mwaka huu ni kilimo, viwanda, majengo na ujenzi.