Home | Terms & Conditions | Help

January 22, 2025, 2:05 pm

Report: Maleria yateketeza zaidi ya watu 429,000 Barani Africa

Nigeria:Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti jana kuwa ugonjwa wa Malaria bado unauwa mamia ya maelfu ya watu hususan katika nchi za kiafrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.


Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo iliyochapishwa jana, mapambano dhidi ya ugonjwa huo yamefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi tangu mwaka 2010. zipo nchi zinazoongoza kwa kuwa na Ueneaji wa ugonjwa huwa ambazo ni Nigeria, Demokrasia ya Congo, Mozambique , Burkina Faso na Sierra Leone


Katika ripoti hiyo WHO imetoa tahadhari kwamba mafanikio hayo yanaweza kudhoofika kutokana na upungufu wa fedha zinazotolewa na jamii ya kimataifa kupambana na Malaria. Mnamo mwaka 2015 watu milioni 212 waliambukizwa Malaria, na 429,000 miongoni mwao walipoteza maisha. Ugonjwa wa Malaria ni kitisho hasa kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5. Ripoti ya WHO inaonyesha kuwa takriban asilimia 70 ya watu wanaouawa na Malaria, ni watoto