- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RC MAKALLA: MARUFUKU WAMACHINGA KUFANYA BIASHARA BARABARANI
Dar es salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amepiga marufuku watu kufanya biashara kwenye maeneo ambayo ni karibu ya barabara zote za Mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo hii leo Septemba 9, 2021 alipotembelea Soko la Kariakoo na kujionea kero ya ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.
Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya September 13 na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia hifadhi ya Barabara.
Aidha RC Makalla amewaelekeza kuangalia utaratibu mzuri wa kufunga na kufungua baadhi ya mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara kutokana na ufinyu wa maeneo ili waweze kupata riziki.
RC Makalla amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini hali ya ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.