Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:43 pm

RC MAKALLA AWAPA POLISI SIKU 7 KUDHIBITI BIASHARA YA NGONO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amempa siku saba Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti watu wote waojihusisha na biashara ya Ngono kwenye eneo la Manzese Uwanja wa Fisi, mara baada ya biashara hiyo kulalamikiwa na Wananchi waliowengi.

Malalamiko hayo yametolewa hii leo Septemba 22, 2021 na wananchi wa Kinondoni wakati wa Mwendelezo wa ziara ya RC Makalla ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni ambapo wamedai kuwa imefikia hatua biashara hiyo inahusha pia utumikishaji wa kingono kwa watoto wadogo Jambo ambalo ni kinyume na sheria na maadili.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Jeshi la Polisi kuwatuma askari watakaovaa nguo za Kiraia na kuwanasa watu wote wanaofanya biashara ya ngono.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa kata na Mtaa huo kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kumaliza suala hilo.