- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS SAMIA: WALICHUKULIA UKIMYA WANGU KAMA UDHAIFU WANGU
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa katika kipindi chake cha miezi sita ya Urais alijaribu kuwa mkimya na mtulivu, kwasababu alikuwa akifanya kazi ya kuzisoma Wizara zote.
Amesema kuwa katika kipindi hicho wapo Mawaziri, Naibu Waziri na Makatibu Wakuu ambao walichukulia ukimya huo kama udhaifu wake.
“yapo mengi ya kurekebisha, wapo pia ambao wakati nawasoma nao wakanisoma, wapo waliochukulia ukimya wangu na utulivu wangu kama udhaifu na wengine wakafanya kazi nzuri”
Kauli hiyo ya Rais Samia imeitoa hii leo Septemba 13, 2021 wakati akiwaabisha viongozi mbalimbali aliyowaabisha leo Jumatatu Ikulu ya Dodoma.
“Mawaziri wapya natumaini mtakwenda kufanya vizuri, uteuzi wenu hauna maana nyie ni wazuri kuliko waliokuwepo uzuri wenu utaonekana katika kazi, hata tuliowateua mwanzo walikuwa wazuri, nataka kuona matokeo sitaki kuwaona kwenye TV tu mnafanya hili mnafanya lile”
“Kipindi cha miezi sita ya Urais wangu nilikuwa najifunza, katika Uongozi kuna mbinu nyingi, Serikali yetu itaendeshwa na matendo makali na sio maneno makali, matendo makali sio kupigana mikwaju ni kwenda kwa Wananchi kutoa huduma inayotakiwa kila Mtu kufanya wajibu wake”
“Msitegemee kwa maumbile yangu haya pengine na malezi yangu kukaa hapa nianze kufoka nahisi sio heshima, na kwasababu nafanya kazi na Watu wazima naamini wanajua wanachokifanya, sitokaa nikaanza kufoka kwa maneno, nitafoka kwa kalamu” amesema Rais Samia