- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS SAMIA: VITA VYA UKRAINE VIMECHANGIA MAFUTA KUPANDA BEI
Rais wa Tanzania Samia Hassan amesema vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine vimesababisha bei ya mafuta nchini na Duniani kupanda.
"Eneo la mabadiliko ya kiuchumi kwa kiasi kidogo limechagizwa pia na uwepo wa vita ya Ukraine na Urusi ni eneo la kupanda kwa bei za mafuta"
Aidha Rais Samaia ameongeza kuwa kwa mwenendo wa jinsi mafuta yanavyopanda bei Tanzania "hatutonusurika na bidhaa zote zitapanda bei nauli zitapanda bei, kila kitu kitapanda thamani ya kila kitapanda kwa sababu mafuta yamepanda"
Rais Samia ametoa mtazamo huo hii leo Marchi 8, 2022 katika Kilele cha Siku ya wanawake Duniani.
"Kiuchumi dunia nzima imerudi nyuma na nchi zetu hizi za uwezo wa chini zimerudi nyuma zaidi kwa upande wetu tunashukuru maamuzi tuliyoyachukua ya kutofungiana wakati wa wimbi la kwanza, pili, tatu la Corona wimbi ambalo limeturudisha kiuchumi lakini hatukurudi kwa kiasi kikubwa kama majirani zetu lakini ukichukulia kwa ujumla duniani. Dunia imeyumba kiuchumi kwa kiasi kikubwa.
"Tumeanza kusikia minong'ono maisha yanakuwa magumu sijui kila kitu kinapanda bei wanasema ni viongozi tulionao, hawana baraka. Sio baraka ya viongozi ni hali ya ulimwengu inavyokwenda mafuta yanapanda bei Duniani na bidhaa zote zinapanda bei" Rais Samia Suluhu Hassan