November 23, 2024, 8:48 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS MAGUFULIA AWAHAKIKISHIA WANANCHI UCHAGUZI HURU NA HAKI
Rais wa Tanzania, John Magufuli amevihakikishia vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2020 kuwa utakuwa huru na wa haki.
Rais amebainisha hayo Jana Juni 16, 2020 wakati akitoa hotuba ya kuvunja Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
Amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu kama ilivyokuwa kwa chaguzi zingine zilizopita unakuwa wa uhuru na haki. “Tutasimamia uhuru na haki wa vyama vyote, na hii ndiyo demokrasia ya kweli, kwa sababu hiyo navisihi vyama vya siasa na wanasiasa kujianda vizuri kushiriki kwenye uchaguzi huu,” amesisitiza Rais Dkt. Magufuli.