Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 3:35 pm

RAIS MAGUFULI: UTUMBUAJI MAJIBU BADO UNAENDELEA

Rais wa Tanzani John Magufuli leo hii Novemba 13, 2020 amelihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa Bunge la 12 la nchi hii.


katika Hotuba yake ya leo Rais Magufuli ameahidi kuimarisha utawala bora hasa kusimamia nidhamu katika utumishi wa Umma pamoja na kupambana na ufisadi, wizi , rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma.

" Kwenye miaka mitano iliyopita tuliwachukulia hatua za kinidhamu watumishi 32,555 na kuiwezesha nchi yetu kushika nafasi ya kwanza kati ya nchi 35 za Afrika kwa kupambana na rushwa, kwa mujibu wa Transparency International na pia kushika nafasi ya 28 kati ya nchi 136 duniani kwa matumizi mazuri ya fedha za Umma kwa mujibu wa utafiti wa Jukwaa la uchumi la dunia (World economic forum) wa mwaka 2019." Alisema Magufuli.053ab1d77d-img20201113113748.jpg

Hata hivyo, Magufuli amesema kuwa watumishi wazembe, wala rushwa, wezi na wabadhirifu wa mali za Umma bado wapo, hivyo amesema miaka mitano ijayo ataendelea kushughulikia suala hilo.

"Na kwa kifupi niseme, utumbuaji wa majipu utaendelea'' alisema

Aidha Rais Magufuli amemuahidi Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itafanya kazi kwa karibu sana na Serikali ya Zanzibar ili kuleta maendeleo kwa pande zote mbili za Muungano.

"Katika hilo ninaahidi kushirikiana kwa ukaribu sana na Rais mpya wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi. Kamwe hatutakuwa na mzaha na yeyote mwenye kutaka kuhatarisha amani ya nchi yetu. Mwenye nia ya kuvuruga umoja na mshikamano wetu, pia mwenye kutaka kutishia uhuru wetu, Muungano pamoja na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar." alisema Rais Magufuli.