- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
RAIS MAGUFULI: NITACHELEWA KUUNDA BARAZA LA MAWAZIRI KWA MIEZI MITATU AU MINNE
Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kuwa atachelewa kuunda baraza la Mawaziri kwa miezi isiopungua mitatu au minne kutokana na Sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi.
Rais Maguguli ametoa kauli hiyo hii leo Novemba 16, 2020 kwenye hafla fupi ya kumuapisha Waziri mkuu wa nchi hiyo Kassim Majaliwa na Mawaziri wawili(Waziri wa Fedha na Mpango Dkt Philip Mpango na Waziri wa Mambo ya njee na Ushirikiaano wa Afrika mashariki Prof. K. Kabudi)
Rais Magufuli amesema sababu kubwa ya kuwateua mawaziri wawili na kuapisha ni kutaka kuwepo na mtu atakayeweza kupanga na kulipa mishahara ya wafanyakazi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Fedha na Mipango, na Waziri wa Mambo ya njee na Ushirikiano wa Africa Mashariki ili kupata msemaji wa mambo ya njee.
“Kwakuwa nitachelewa kidogo kwa miezi mitatu, minne kuunda Baraza la Mawaziri nikasema tuwe na Waziri wa Fedha na kwenye Mambo ya Nje nikaona hatuwezi kosa Mtu wa kutusemea Watu wakitutukana tukakosa majibu nikaona huyu Kabudi kwa kuwa alimudu nafasi yake acha aendelee”
“Mawaziri wawili niliowateua sio kwamba ni maarufu sana kuliko waliobaki, nimeona kwa sababu nitachelewa kidogo kuwa na Baraza la Mawaziri na Wabunge lazima mlipwe posho na mishahara nikasema lazima tuwe na Waziri wa Fedha maana hatuwezi kusubiri miezi yote mitatu au minne” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia amewataka wabunge wote wa chama chake waliochaguliwa waondokane na haraka ya uteuzi kwakuwa Wabunge hao waliomba kwa wananchi nafasi za Ubunge na Si Uteuzi wa waziri au naibu waziri.
"Ningewaomba waheshimiwa wabunge presha mzishushe kwa sababu kazi mliyoomba ni ubunge sasa haya mengine yanatoka wapi?"- amesema Rais Magufuli.
“Mlikwenda kuomba Ubunge kwamba mtawatumikia Wananchi wenu, sasa mengine yanatoka wapi!?, nafasi za Mawaziri na Manaibu Waziri huenda hazitofika 30, katika Watu 350 hata ungekuwa wewe unateua ungepata shida kubwa lazima ucheki jina kwa jina, tuwe na subira”