- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
PROF. LIPUMBA: RAIS SAMIA ASISUBIRI MAANDAMANO YA KUDAI KATIBA MPYA
Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amemsihi Rais wa sasa wa Tanzania Bi Samia Suluhu Hassan kuwa asisubiri maandamano kufanyika ya kudai tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya ndio aanze mchakato na badala yake anapaswa kuanza sasa kabla ya hayo kutokea.
Lipumba amesema kwakuwa Samia alikuwa Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba, kwahiyo anaelewa vizuri kinaga ubaga umuhimu na mambo yaliyopo kwenye katiba ile.
"Kwa kuwa yeye (Rais Samia Suluhu Hassan) alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, kwa hiyo anajua mambo yalivyojaidiliwa. Ni matarajio yangu ataona umuhimu wa suala hili, na kwamba asisubiri maandamano ya kudai Tume Huru na Katiba Mpya". - Prof. Ibrahim Lipumba
Aidha, Prof. Lipumba asema Rais Samia ana kipaji cha lugha ya Kiswahili na Kiingereza na lugha laini aliyoiita ya kumtoa nyoka pangoni kwa kuwa kauli zake ni za kutia matumaini wananchi iwapo aliyozungumza katika hotuba yake yatatekelezwa basi nchi itapiga hatua.
"Mtu anaweza kusema kwamba CCM ni ile ile lakini kwangu la muhimu ni kupima vitendo vya Rais Samia kama atatembea kwenye maneno yake naamini kama chama tunaweza kupata fursa ya kueleza sera zetu za haki sawa na furaha kwa wote