Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 12:43 pm

POLISI ZANZIBAR: ZAINAB ALIKUWA NA USHAHIDI WA KUBUMBA

Zanzibar. Kamanda wa Polisi Mkoa wa kaskazini Unguja Kamishna Msaidizi wa Polisi Martin Leo Otieno amesema kesi iliyoripotiwa na Raia Mmoja wa Nigeria anayafahamika kwa jina la Zainab Oladehinde raia wa Nigeria Ilikosa mashiko ya kufikishwa mahakamani kwasababu ya Kukosekana Ushahidi madhubuti.

Kamanda Martin ameeelza hayo wakati akizungumza na Vyombo vya habari makao makuu ya Polisi Zanzibar, amesema kesi hiyo ya kudhalilishwa ambayo iliripotiwa April 18, 2021 na Raia mmoja wa Nigeria ambae alikua Zanzibar kwa mapumziko ya kawaida huko katika hotel ya Warere iliyopo Nungwi ndani ya Mkoa huo na kudai kuwa alidhalilishwa na mmoja ya mvulana ambae aliingia chumbani kwake alipokua katika hotel hiyo

Kamanda Martin Amesema kesi hiyo baada ya kufanyiwa upepelezi jarada lilifikishwa ofisi ya DPP na kushindwa kufikishwa mahakamani baada ya ofisi ya DPP kutoridhishwa na ushahidi uliotolewa ambapo Raia huyo wa Nigeria alisema anamtambua mtuhumiwa kwa harufu

Hii inakuja siku chache baada ya Raia huyo wa kigeni wa Nigeria kusambaa taarifa ya kufanyika kwa tukio hilo ambalo kwa mujibu wa taarifa tukio hilo limefanyika Mwaka jana