Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 10:12 pm

POLISI DODOMA: MBOWE AMEVUNJWA MGUU WA KULIA

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limesema kuwa wamepata taarifa ya kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alivamiwa na watu wasiojulikana na wamemkuta ameumizwa na kuvunjwa mguu wa kulia.

Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi imetolewa asubuhi ya Leo Juni 9, 2020 na Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Giles Muroto

"Zipo taarifa kwamba Mhe.Mbowe amevamiwa na watu watatu wakamkanyaga kanyaga na kumvunja mguu wa kulia" amesema Muroto

Kamanda Muroto amesema wanaendelea na uchunguzi juu ya swala hilo la kushangaza "lakini tunafuatilia tutatoa taarifa baadae..hali yake ni nzuri tu". amesema Kamanda wa Polisi Dodoma-Giles Muroto.

Taarifa za chama chake chadema zimesema kuwa mbowe alivamiwa usiku wa kuamkia leo Juni 9, 2020 alipokuwa anatoka katika shughuli za kikazi na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya General mjini Dodoma.