Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 4:54 pm

POLISI DAR: PADRI KANGWA HUENDA AMEJIUA MWENYEWE

Dar es salaam. Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiuchunguzi wamesema uchunguzi wa awali wa kifo cha Padri Francis Kangwa kinaonesha huenda amejiua mwenyewe kutoka na sababu mbalimbali.

Aidha Polisi wamesema wanaendelea kuchunguza kwa kina kifo cha Padri huyo Raia wa Zambia aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mbezi Mshikamano iliyopo Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es salaam aliyekutwa amefariki ndani ya Tenki kubwa la maji lililoko nyuma ya nyumba ya makazi ya Mapadri iliyopo Mtaa wa Sokoine katika jengo la Ottoman, Jijini hapa .

"Padri huyo alifika katika Kanisa la 'St. Joseph' lililopo Mtaa wa Sokoine tarehe April 12,2022 kwa ajili ya ibada maalum, na mara baada ya ibada alielekea kwenye makazi ya Mapadri kujipumzisha lakini hakuonekana mpaka tarehe April 15,2022 alipokutwa amefariki eneo hilo"

"Uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiuchunguzi unaonesha dalili kwamba Padri huyo anaweza kuwa amejiua, hata hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi iliyopelekea kifo cha Padri huyo"